Serikali imepiga marufuku kuweka plastiki laini kufunikia vifuniko vya chupa za vinywaji vyote vinavyozalishwa Tanzania bara na vinavyoingizwa nchini kutoka nje ya Tanzania bara baada ya miezi sita kuanzia leo Oct 11, 2021 huku Ikiwaelekeza wazalishaji wa vinywaji baridi kuanza uzalishaji wa bidhaa hizo kwa kuzingatia umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa kutokuweka plastiki laini nje ya kifuniko cha chupa.
"Baada ya muda huo wa miezi sita kumalizika, wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa hizo wanaelekezwa kuzalisha bidhaa zao bila kuwa na plastiki laini zinazofunika vifuniko vya chupa hizo, bidhaa zilizozalishwa na kuingia sokoni kabla ya katazo hili ambazo muda wa mwisho wa matumizi (expiry date) haujafika, zitaendelea kubaki sokoni hadi pale muda wake wa matumizi utakapoisha"
"Bidhaa zote za vinywaji baridi zenye plastiki laini zinazofunika kifuniko cha chupa zitakazozalishwa baada ya miezi sita kuanzia tarehe ya tangazo hili, hazitaruhusiwa kuingia sokoni"
"Wazalishaji wa bidhaa za vinywaji vyenye plastiki laini kwenye kifuniko cha chupa waige mfano wa wazalishaji wa bidhaa za maji, juisi na soda ambazo haziwekwi plastiki laini kwenye kifuniko, Stempu za Kielektroniki za TRA (TRA Electronic stamps) ziendelee kutumika kutambulisha uhalali wa bidhaa zetu nchini",,,JAFO
No comments:
Post a Comment