Friday, August 28, 2020

Lionel Messi Kutaka kuondoka Barcelona


 Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi mwishoni mwa wiki amewasiliana na meneja wa Man City, Pep Guardiola na kumfahamisha kwamba anataka kuondoka Barcelona.

Manchester City inaweza kuwatoa mabeki wake raia wa Hispania Eric Garcia, 19, na Angelino, 23, kama chambo ili kumnasa Messi, kama hawatamsainisha akiwa mchezaji huru.Manchester City inajiandaa kuipa Barcelona kitita cha £89.5m pamoja na Garcia, kiungo wa Kireno Bernardo Silva, 26, na mshambuliji wa Brazil Gabriel Jesus, 23, kwa ajili ya kumnasa Messi.

No comments: