Friday, August 21, 2020

MCHUNGAJI MAARUFU NIJERIA HUYU APA

 

Enoch Adeboye, anayefahamika zaidi kama "Daddy Go" (Baba Msimamizi Mkuu), ni mchungaji wa Nigeria anayependwa na mamilioni ya wafuasi wake, lakini ambao pia wamekua wakimkosoa kwenye mitandao ya kijamii kwa kile wanachosema ni hurka yake ya ubaguzi wa kijinsia.

Mchungaji huyo mwenye umri wa miaka 78- aliwekwa katika kiwango cha wachungaji wenye mapato ya chini miongoni mwa wachungaji matajiri wanaotoa mahubiri kwa njia ya televisheni katika taifa hilo lililoko magharibi mwa Afrika, lakini amekua maarufu sana.

Amekuwa mkuu wa kanisa linalofahamika kama Redeemed Christian Church of God (RCCG) kwa karibu 40 - na chini ya uongozi wake thabiti kanisa hilo limekuwa kwa kiwango kikubwa.

Ni nadra kuupata mtaa wa eneo la kusini mwa Nigeria linalokaliwa na Wakristo wengi bila kanisa la RCCG, baadhi ya mitaa hata huwa na makanisa mawili-na nembo yake ya njiwa imekuwa ni sehemu ya utambulisho wake.

Lakini maoni ya mchungaji juu ya ndoa na majukumu ya kijinsia yamekuwa yakiwashangaza baadhi ya watu katika enzi hii ya age kampeni ya #metoo - hata katika taifa hili lenye itikadi.

No comments: