Saturday, September 5, 2020

IFAHAMU iOS 13.7 YA APPLE


Apple ametoa iOS 13.7 kwa watumiaji wote wa iPhone. Update hii mpya, Apple ameweka features mpya katika Settings na Notifications za Corona. Kama unakumbuka Apple alikuwa anatengeneza uwezo wa Simu kuwa na App ya kukujulisha kama umekaribiana na mtu ambaye ana Corona kwa kutumia Bluetooth, GPS, ID ya Simu na app ambazo zitakuwa zinatengenezwa na nchi na taasisi mbalimbali kusaidia kutoa taarifa ya historia ya mtu kupata Corona.⠀

⁣⁣𝗶𝗢𝗦 𝟭𝟯.𝟳⠀
✺ Apple ameweka sehemu maalum katika settings inayohusu “Exposure Notifications” ambayo itaunganishwa na applications zinazotumia ku-track Corona.⠀

✺ Unaweza ku-share link ya file lililopo katika app ya “Files” ambayo inaunganishwa na iCloud Drive yako. ⠀

✺ Maboresho machache katika security.⠀

Pia updates mpya ni kuwa, iOS 14 itatoka mwezi huu, japo ilipangwa itoke pamoja na iPhone 12 lakini kutokana na changamoto chache ambazo Apple anapambana nazo katika screen 120Hz na issue ya Corona, Apple atatoa iPhone 12 October na iOS 14 itatoka mwezi huu na iPad Air Mpya na Apple Watch 6.⠀
 

No comments: