Microsoft ilitangaza katika tovuti yake kuzindua “Microsoft Video Authenticator” ambayo ina uwezo wa kuhakiki picha na video na kutoa asilimia kuonyesha kiwango cha video au picha kubadilishwa na kutoa hitimisho kama video au picha ilibadilishwa. Mfumo huo pia una uwezo wa kutambua sura ambayo imebadilishwa, mdomo unavyocheza, na kutofautisha rangi asilia ya video na ambayo imebadilishwa. Teknolojia hii itatambua endapo ukiwa umebadilisha sura za wahusika katika picha na video.
Microsoft imefungua tawi lake jipya la Project Origin na ataanza kushirikiana na baadhi ya kampuni kuanza kutumia mfumo huo. Ni wazi kuwa Microsoft imeona biashara hii ya mfumo wa kuhariri video na picha ambazo zimebadilishwa ni nafasi nzuri ya kibiashara katika kizazi cha sasa ambacho kinatumia filters, emoji, applications za kubadilisha sura na ubunifu wa aina mbalimbali.

No comments:
Post a Comment