Uchunguzi umeanzisha na Shirikisho la soka la Misri FA (EFA) baada ya kubaini kuwa vikombe kadhaa vimepotea kutoka makao makuu yake mjini Cairo, likiwemo kombe asili la Mataifa ya Afrika.
Misri ilipokea zawadi ya kombe hilo iposhinda michuano ya 2010, kwa kuwa ilikuwa imeshinda kombe la aina hiyo kwa mara ya tatu.
Kombe hilo ambalo mtindo wake ulitumiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002 baada ya Cameroon kupewa kombe la awali baada ya kushinda mara tatu shindano hilo, lilitolewa kwa EFA na shirikisho la soka la Afrika (Caf) baada ya kupata ushindi mara tatu mwaka 2006, 2008 na 2010.
Ijumaa Shirikisho la soka la Misri EFA - ambalo mkurugenzi wake wa habari aliithibitishia BBC kupotea kwa kombe hilo - alisema wameanzisha uchunguzi juu ya kupotea kwa vikombe mbalimbali.
"Wakati Chama cha Soka cha Misri kwa sasa kinafanya ujenzi makao yake makuu , ikiwa ni pamoja na kubadilisha lsehemu ya lango kuu la kuingia kwenye makumbusho madogo ya soka ya Misri, utawala wake umeshitushwa na kupotea kwa baadhi ya vikombe katika chumba maalumu cha kuhifadhia vikombe ," taarifa ya EFA imesema.
Baada ya kushambuliwa kwa makao makuu ya EFA mwaka 2013, vikombe mbali mbali -likiwemo Kombe la Mataifa ya Afrika -vilihamishiwa kwenye chumba kingine maalum.
No comments:
Post a Comment