Saturday, September 5, 2020

MTOTO WA RAISI WA NIGERIA AOLEWA

 


Mke wa rais wa Nigeria Mahammadu Buhari,-Aisha Buhari ametuma picha za harusi ya binti yake Hanan na mkwe wake Mohammed Turad kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Alituma wa picha iliyoambatana na ujumbe ''HamadForever Alhamullilah'' akimaanisha ''HamadDaima Alhamdullilah''

Ilikuwa imeripotiwa kwenye mitandao ya kijamii tangu mwezi Agosti kwamba binti wa Rais Muhammadu Buhari, Hanan, ataolewa na mtoto wa kiume wa mwanasiasa maarufu kutoka jimbo la Kaduna Sani Sha'aban Mohammed Turad.

Harusi yao ya kufana imefanyika jana katika kasri la Aso rock.

Muhammad Turad Sha'aban, ni mtoto wa kiume wa mbunge wa zamani wa Nigeria aliyewakilisha jimbo la Sabon Gari Zaria katika bunge la 5 la taifa la Nigeria, aligombea ugavana katika uchaguzi wa mwaka 2007 na wa mwaka 2011.

Alhaji Sani Sha'aban ana mamlaka ya jamii ya ÆŠamburam katika ufalme wa Zazzau.

Taarifa zinasema kuwa Turad ni mtaalamu wa masuala ya fedha.

No comments: