Saturday, September 5, 2020

HISTORIA YA OTA BENGA


 Ota Benga alitekwa nyara kule ambako sasa hivi kunafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1904 na kupelekwa Marekani lengo likiwa nikumfanya kuwa onyesho.

Mwanahabari Pamela Newkirk, ambaye ameandika mengi kuhusu suala hilo, anaangalia matukio kadhaa ya kuficha ukweli wa kile kilichotokea.

Zaidi ya karne moja baada ya suala hilo kuangaziwa kimataifa kwa kumuonesha mwanaume kijana Mwafrika katika makazi ya nyani, Bustani ya Wanyama ya Bronx, mji wa New York hatimae imeonesha masikitiko yake.

Shirika la kuhifadhi Wanyama pori limeomba msamaha kwa onesho la mwaka 1906 la kumuonesha Ota Benga, mzaliwa wa Congo, hatua iliyokuja baada ya maandamano duniani yaliyosababishwa na video inayoonesha mauaji ya George Floyd na kuanza tena kuangazia ubaguzi unaotokea Marekani.

Wakati Marekani inakumbana na maandamano hayo, Cristian Samper, Rais wa chama cha uhifadhi wa wanyama pori, alisema ni muhimu "kuakisi historia ya hifadhi hiyo na ubaguzi wa rangi katika taasisi zetu".

Aliapa kwamba bustani ya wanyama ya Bronx, itahakikisha kwamba inakuwa na uwazi kuhusu kile kilichogonga vichwa vya habari kote Ulaya na Marekani kuanzia Septemba 9, 1906 siku moja baada ya Ota Benga kuoneshwa kwenye onesho hadi alipoondolewa kwenye bustani hiyo. Septemba 28, 1906.

'Alikuwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo'

Badala ya kujikita kwenye mafunzo waliopata, Shirika hilo la uhifadhi wa wanyama pori limejihusisha na walivyoficha ukweli kwa karne nzima kipindi ambacho lilishindwa kuweka sawa au kuzungumzia kile ambacho hasa kilikuwa kimetokea kwa mwanaume huyo mweusi.

Mapema mwaka wa 1906 barua kutoka kwa hifadhi hiyo inaonesha kwamba wakati ukosoaji wa kitendo hicho unaendelea, maafisa waliamua kuanzisha taarifa za uongo kwamba Ota Benga alikuwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo.

2px presentational grey line

Ota Benga alikuwa nani?

  • Alikamatwa Machi 1904 na mfanyabiashara wa Marekani Samuel Verner kutoka kule ambako kulikuwa kunafahamika kama Congo ya Ubelgiji. Umri wake haujulikani, pengine alikuwa na miaka 12 au 13
  • Alisafirishwa kwa meli hadi New Orleans na baadae mwaka huo aliwekwa kwenye maonesho ya Dunia huko St Loius na vijana wengine wanane
  • Maonesho hayo yaliendelea hadi miezi ya baridi ambapo kundi hilo halikupewa nguo za kujikinga na wala malazi.
  • September 1906, aliwekwa kwenye maonesho kwa siku 20 katika bustani ya wanyama ya Bronx huko New York na kuwa kivutio cha wengi kufika katika eneo hilo.
  • Ghadhabu kutoka kwa mawaziri wa Kikristo ilitamatisha kushikiliwa kwake na alihamishwa hadi hifadhi ya yatima weusi ya Howard New York iliyokuwa inasimamiwa na mchungaji Mmarekani Mweusi James H Gordon.
  • Januari 1910 alienda mji wa Lynchburg. Seminari ya kitheolojia kwa wanafunzi weusi huko Virginia.
  • Huko alifunza wavulana waliokuwa jirani namna ya kuwinda na uvuvi pamona na kuwasimulia kilichomtokea nyumbani.
  • Baadae alisemekana kwamba amepata ugonjwa wa sonona kutokana na kutamani nyumbani kwao na Machi 1916 akajipiga risasi kwa bunduki ambayo alikuwa ameificha. Inadhaniwa kwamba wakati huo alikuwa na umri wa karibu miaka 25.

Chanzo: Spectacle: Maisha ya kushangaza ya Ota Benga)

2px presentational grey line

Mwaka 1916, baada ya kifo cha Benga, makala ya gazeti la New York ilifuta simulizi ya maonesho yake.

"Kazi hii ndio chanzo cha kujulikana kwa taarifa ambayo ilikuwa iliyofichwa na hifadhi ya wanyama pori kuwa alikuwa akishikiliwa kwenye hifadhi kama mmoja wa waliokuwa wakifaniwa maonesho kwenye kizimba cha nyani. Makala hayo yameeleza.


Makala hayo ilikinzana na nyingine nyingi zilizotolewa miaka kumi ya awali katika magazeti mbalimbali kote nchini humo na Ulaya.

Gazeti la New York Times pekee lilikuwa limechapisha taarifa kadhaa kuhusiana na suala hilo, moja wapo ikiwa ni Septemba, 9 1906, ambayo kichwa cha habari kilikuwa: " Bushman Shares A Cage With Bronx Park Apes". Yaani 'Mtu wa porini aishi na nyani kwenye kizimba kimoja kwenye hifadhi ya Bronx'

Kisha, mwaka 1974, William Bridges, mtunzi wa hifadhi hiyo alidai kwamba huenda kile hasa kilichotokea kisifahamike.



(@BBCSWAHILI)


No comments: