Thursday, December 10, 2020

WATANZANIA WATIMBA MTV MAMA AWARDS 2020



Watoto watano wa ‘JPM’ wamechaguliwa 
kuwania Tuzo za MTV Mama Awards ambazo zitatolewa Kampala Uganda mwanzoni mwa mwaka 2021.

ROSTAM ambao ni @staminashorwebwenzi na @roma_zimbabwe wanawania Tuzo ya Kundi Bora Afrika wakiishindani hiyo Tuzo na Sauti Sol, Ethic, Calema, Kabza de small na Dj Maphorisa, pia Blaq Diamond
Zuchu @officialzuchu anawania Tuzo ya Breakthrough Act akiwa na Tems, Sha Sha, Omah Lay, John Blaq, Focalistic na Elaine.

Harmonize @harmonize_tz anawania Tuzo ya Msanii Bora wa kiume akiipambania na Burna Boy, Fireboy DML, Innoss’B, Kabza de Small, Master KG na Rema.

Simba Diamond Platnumz @diamondplatnumz anaiwania Tuzo ya Msanii bora wa mwaka kwenye kipengele kimoja na Burna Boy, Calema, Davido, Master KG, Tiwa Savage na Wizkid. 

Hongera sana kwa Wakali wetu wote kwa kuchaguliwa kwenye hizi Tuzo kubwa za Afrika, All the best kuipeperusha 🇹🇿!!


 

No comments: