Thursday, October 14, 2021

Streams za Boomplay Kuingizwa Billboard Charts


Kama sehemu ya kuendelea kusaidia tasnia ya muziki wa Afrika kutanua wigo wake, Boomplay imetangaza rasmi, sasa itaingiza kazi za wasanii katika chati maarufu za Billboard Hot 100, Billboard 200, Artist 100 na Billboard Global 200, na pia chati zingine zote za Billboard Marekani na kimataifa ambazo zinajumuisha kazi za kupakua na kusikiliza muziki.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na Kampuni ya Transsnet Music Limited ambayo ndiyo inayomiliki Programu tumuishi (App) ya Boomplay, kazi itaanza rasmi kuanzia wiki ya (Oktoba 15-21) chati za Billboard za Oktoba 30).

Aidha, pamoja na mamilioni ya nyimbo za Kiafrika kusikilizwa kupitia programu hiyo duniani kote, kujumuishwa kwa taarifa za Boomplay katika chati hizo kubwa za muziki kunawapa wasanii wa Kiafrika na Kimataifa na muziki uliopo kwenye program hiyo fursa ya kuonekana zaidi kwenye majukwaa makubwa duniani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndani ya jukwaa la Music Connect la MRC Data, kazi za Boomplay zitajumuishwa kwenye kapu moja la takwimu linalojumuisha mahitaji ya sauti na picha ambapo picha zimeanza kuonekana kuanzia Oktoba 12, 2021 na miito Oktoba 8, 2021.

Kwa mujibu wa Billboard, "msingi wa takwimu za MRC umejengwa juu ya kuipa tasnia ya muziki na wateja wetu maoni kamili zaidi ya utumiaji wa muziki. Tunafurahi kutangaza takwimu za ziada zitakazopatikana kutoka Boomplay," imeeleza.

Mkurugenzi wa Maudhui na Mkakati wa Boomplay, Phil Choi amebainisha kuwa: "Kuingia kwa Boomplay kwenye chati hizi ni hatua muhimu katika kuhakikisha wasanii wa Kiafrika wanawakilishwa na wanapata fursa sawa kama wanazopata wasanii wa kimataifa. Jambo hili linawezekana kuonekana gumu hapo awali, hivi sasa tunaweza kusema tumefika kufuatia ushirikiano wetu na chati za Billboard,"

Streams za Boomplay ziliizoingizwa kwenye chati za Billboard zinawakilisha streams kutoka kwa wasikilizaji waliojisaliji kawaida na wale wa kulipia huku kila stream kutoka kwa msikilizaji wa kundi husika vikipimwa kwa uzito wake.(@boomplaymusic_tz )

No comments: