Monday, October 11, 2021

Watu wenye Magonjwa Kiakili Kujiajiri


SERIKALI imeombwa kuweka utaratibu wa kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kujitegemea watu wenye magonjwa ya akili kutokana na vitendo vya ukatili wa kutumikishwa na kupewa ujira mdogo wanavyo tendewa katika jamii. Baadhi ya wana jamii mkoani Kigoma wamekuwa wakiwatumia wagonjwa wa akili katika shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo,uzalishaji wa viwanda vidogo na ubebaji mizigo ili kujinufaisha wao . Noela Paulo mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji amesema serikali inapaswa kuweka mfumo wa kuwabaini watu hao na kuweka mfumo wa kuwawezesha ili waweze kujisimamia na kuepukana na vitendo hivyo. Amesema pia inapaswa hatua za kisheria dhidi ya wanaotenda ukatili huo kuchukuliwa ili kukomesha vitendo vya aina hiyo kwenye jamii.

No comments: